↧
PICHA ZA MAZISHI YA KADA WA CHADEMA IRINGA ZITAKUJIA HIVI PUNDE MTANDAO UNASUMBUA LEO
↧
ZIARA YA KINANA MKOANI TABORA
Pichani Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora,Ndugu Hassani Wakasubi akimpokea mgeni wake,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo katika kijiji cha Makomelo wilayani Igunga mkoani Tabora kwa ziara ya siku 10,ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.
Ndugu Kinana akisalimiana na Wananchi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Makomelo mapema leo jioni.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama ngoma ya kiasili iliondaliwa wilayani Igunga wakati wa mapokezi ya Ndugu Kinana, ambaye ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa chama hicho,mara baada ku kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani hummo jioni ya leo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.
Ndugu Kinana akipokelewa na vijana wa Green Gard tayari kwa kuvalishwa skafu na kukaribishwa wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.
Baadhi ya wananchi mbalimbali waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo Wilayani Igunga mkoani Tabora.
Sehemu ya magari ya Wenyeji waliofika kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana jioni ya leo katika kijiji cha Makomelo,wilayani Igunga mkoani Tabora jioni ya leo.
Ndugu Kinana akivalishwa skafu
Ndugu Kinana na Ujumbe wakiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wilayani humo,kwa ajili ya kikao kupata taarifa ya maendeleo ya wilaya na mkoa sambamba na hali ya siasa.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Kamati ya Siasa na Mkoa wakiwa kwenye kikao hicho,ambapo Ndugu Kinana pia alizungumza nao.
PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA-IGUNGA TABORA
↧
↧
WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAPEWA SEMINA YA KUELIMISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi Mkuu wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Julius Ningu akifungua mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari juu ya utunzaji wa Mazingira na kuelekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani mapema mwezi wa Sita.
![]()
Mwendesha mada wakati wa Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari juu ya masuala ya mazingira Bi. Singlunda akitoa maelezo na mwongozo wa mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.
Mmoja ya Wataalam wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira akifafanua Jambo juu ya Siku ya Mazingira Duniani wakati wa Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari juu ya masuala ya Mazingira
Bi. Matha Ngolowera Afisa Elimu Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais akifafanua Jambo juu ya Tuzo ya Rais Dr. Jakaya Kikwete ya Upandaji wa Miti ambayo hutolewa mara moja kwa mwaka wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
Bi. Fainahappy Kimambo Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akisisitiza Jambo kuelekea siku ya Mazingira Duniani.
Injinia Ladslaus Kyaruzi Mhandisi Mwandamizi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akitoa mada juu ya Mabadiliko ya tabia Nchi.
Baadhi ya wahariri wa vyombo Mbalimbali vya Habari wakiwa katika mkutano wa Mafunzo ya Masuala ya Mazingira wakati wa kuelekea siku ya Mazingira Duniani mapema mwezi ujao.
↧
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MFANYABIASHARA MAARUFU WA NIGERIA ALHAJ ALIKO DANGOTE JIJINI ABUJA



PICHA NA IKULU
↧
Serikali ya Tanzania yasaini msaada wa zaidi ya Sh. Bilioni 134 kusaidia sekta ya kilimo na usafirishaji.

(Picha na Wizara ya Fedha)

………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
SERIKALI ya Tanzania imetiliana saini mkataba wa msaada wa zaidi ya Shilingi Bilioni 134 sawa na Euro milioni 59.5 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kusaidia sekta ya kilimo na usafirishaji nchini.
Mkataba huo ulisainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa EU nchini Filberto Sebregond leo jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya kutia saini mkataba huo, Dkt. Likwelile alisema kuwa sehemu ya msaada huo ambao ni Shilingi Bilioni 82.4 ambazo ni sawa na Euro milioni 36.5 utatumika kuendeleza sekta ya kilimo na kukuza uchumi nchini kwa kupitia kituo maalum cha uendelezaji kilimo ukanda wa Kusini Tanzania (SAGCOT) na kuboresha miundombinu ya barabara za ukanda huo.
Vilevile Dkt. Likwelile alisema kuwa sehemu iliyobaki ya msaada huo ambao ni Shilingi Bilioni 51.9 ambazo ni sawa na Euro milioni 23 itatumika kuimarisha biashara na ushirikiano katika jumuiya kwa kuanzisha kituo cha pamoja cha ukaguzi mipakani (OSIS).
“Vituo hivyo vya ukaguzi mipakani vitakuwa na manufaa si kwa Tanzania tu, bali hata katika nchi mbalimbali zinazopakana na Tanzania” alisema Dkt. Lkwelile.
Alifafanua kuwa msaada uliosainiwa unamanufaa kwa wananchi kwa kuboresha miundombinu vijijini na kusambaza umeme vitu ambavyo vitasaidia kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Naye Balozi wa EU nchini Filberto Sebregond alisema kuwa anaamini msaada huo utasaidia juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuongeza nafasi za ajira, kupungua kwa bei za bidhaa mbalimbali na kuendelea kukuza uchumi nchini.
Balozi huyo alisema kuwa EU inaamini kuwa ushirikiano wake na Tanzania utaendelea kuimarika kwa kuhimiza maendeleo kwa pande zote mbili na amani ya watu wake.
Hafla hiyo ya kusaini mkataba ilihudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Fedha, Nishati na Madini, Uchukuzi na Ujenzi, EAC, DFID, SAGCOT, wajumbe kutoka EU, Shirika la maendeleo ya Ufundi kutoka Ubelgiji na washirika wa maendeleo.
↧
↧
SERIKALI YAKUSANYA BILIONI 3 KUTOKA KATIKA MAKUSANYO YA MRAHAMA WA MADINI NCHINI

……………………………………………………………
Frank Mvungi-Maelezo
SERIKALI imekusanya takribani shilingi bilioni 3 kutokana na kuongezeka kwa makusanyo ya mrabaha uliotozwa katika madini ya Ujenzi katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani katika kipindi cha Juni mwaka 2011 hadi Novemba mwaka 2013.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bruno Mteta wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Mteta alisema awali kabla wakala huo haujaanza ukaguzi wa madini ya ujenzi kiasi kilichokuwa kikikusanywa ni shilingi milioni tatu tu kwa mwaka hivyo kwa sasa kiwango hicho kimefikia wastani wa Bilioni moja kwa mwaka.
Alisema ukaguzi umeimarishwa katika vituo vyote ambavyo wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara hiyo wanalazimika kupita na kuonyesha vibali vya kusafirisha madini hayo ambavyo ni vocha maalum zinazotolewa na wakala huo ili kudhibiti wale wanaokwepa kulipa mrabaha.
“Tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa kila anayetakiwa kulipa mrabaha katika biashara ya madini ya ujenzi anafanya hivyo kwa kuimarisha ukaguzi kupitia vituo vyetu vya Afrikana,Pugu,Chalinze na katika maeneo yote yaliyobainishwa kutumika katika uchimbaji wa madini ya Ujenzi” alisema Mteta.
Katika hatua nyingine Mteta alisema kuwa ni wajibu wa kila mchimbaji na mfanyabiashara wa madini kulipa mrabaha unaostahiki ambapo kifungu cha 87 (6) cha sheria ya Madini ya mwaka 2010 kinachotaka mrabaha ulipwe kwa kuzingatia thamani halisi ya madini (gross value)yanapofikishwa sokoni au kwa mtumiaji.
Naye Mkurugenzi wa udhibiti na Ukaguzi wa Uzalishaji na Biashara ya Madini Mhandisi Liberatus Chizuzu alitoa wito kwa wananchi hasa wafanyabiashara wa madini ya ujenzi kuzingatia sheria na kanuni za Madini ili kulisaidia Taifa kujenga uchumi imara.
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania TMAA kwa kushirikiana na Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Mashariki ulianzisha matumizi ya hati za mauzo ya Madini ya Ujenzi katika ukaguzi wa uzalishaji na mauzo ya madini ya ujenzi Kanda ya Mashariki (Mikoa ya Dar es salaam na Pwani) ambapo matumizi ya stakabadhi hizo yameongeza pato la Serikali kwa kiasi kikubwa kutokana na makusanyo ya mrabaha kwa kiasi kikubwa.
↧
MBUNGE MGIMWA NI SAWA NA SIKIO LA KUFA?
Godfrey Mgimwa mbunge wa Kalenga |
GODFREY MGIMWA, (amezaliwa Agosti 24, 1981) ni mwanasiasa kijana wa Tanzania. Ni mbunge wa nne kuliongoza jimbo la Kalenga Mkoani Iringa baada ya marehemu Steven Galinoma, George Mlawa na baba yake Dk William Mgimwa.
Alishinda kiti hicho cha ubunge Machi 16, 2014 baada ya kujizolea kura 22,962 sawa na asilimia 79.27 ya kura zote zilizopigwa.
Ameapishwa Mei 6, 2014; wananchi wa jimbo lake wana matarajio mengi kutoka kwake; yanahusu ahadi zilizotolewa na chama chake Chama cha Mapinduzi (CCM), marehemu baba yake na za kwake mpya alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi huo.
Ni mtiririko wa ahadi: ni lazima azikumbuke, aoneshe jitihada ya kuzifanyia kazi na azitekeleze katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliobaki kabla watanzania hawajaingia kwenye harakati za Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Sifa moja kubwa aliyokuwa nayo Chifu wa Wahehe, Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga, ambaye alijulikana kwa jina la Chifu Mkwawa, enzi za uhai wake ni ushujaa.
Chifu Mkwawa alikuwa shujaa, hakupenda kuonewa na wala hakupenda kuwabagua watu wake, aliacha historia kubwa ya kupigania haki za Wahehe enzi za utawala wake na hakika alipambana na utawala wa Kijerumani.
Sifa hizo amewaachia wahehe; wanazienzi kwa kupambana na maendeleo yao ya kila siku na ndio maana historia katika jimbo hilo inaonesha wananchi wake hawajali kuchukua maamuzi magumu pale wanapohisi kudanganywa, kuonewa na kubaguliwa katika maendeleo wanayoyataka.
Historia hiyo inatoa changamoto kubwa kwa Godfrey Mgimwa; mwaka mmoja na nusu ni kipindi kifupi kupima utekelezaji wa ahadi zake, lakini kwa kuwa ameahidi, na kaahidi kuzitekeleza kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 ni lazima afanye hivyo ili yasimkute yaliyowakuta baadhi ya wabunge waliotangulia.
Tangu taifa hili liingie kwenye mfumo wa vyama vingi, jimbo hilo ndio jimbo pekee kwa mkoa wa Iringa na Njombe ambalo halijawahi kuwa na mbunge aliyeongoza mfululizo kwa zaidi ya awamu moja ya miaka mitano.
Mwaka 1995 serikali ilipoamua kujiingiza kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi vya siasa, jimbo hilo lilimchagua Steven Galinoma baada ya kuja na ahadi nyingi zilizoonekana kutatua changamoto mbalimbali za wana Kalenga.
Galinoma alishindwa kutekeleza nyingi kati ya ahadi hizo katika sekta ya afya, maji, mawasiliano, kilimo, miundombinu ya barabara, umeme n.k; wananchi wakaamua kumpiga chini katika kura za maoni za mwaka 2000 na kujikuta akiwatumikia wana Kalenga kwa miaka mitano tu tofauti na matarajio yake.
Mwaka 2000, wana Kalenga, wakitumia ujaziri ule ule waliolithiri kutoka kwa Chifu Mkwawa, wakamchagua George Mlawa kuwa mbunge wao. Kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo, Mlawa alikuwa Katibu wa Bunge.
Akapigwa chini mwaka 2005; ni baada ya kushindwa kutekeleza nyingi ya ahadi alizozirithi kutoka kwa mtangulizi wake marehemu Galinoma.
Wananchi wa jimbo hilo wakamrudisha tena Galinoma mwaka 2005; ni baada ya kuahidi kurekebisha makosa aliyoyafanya awamu yake ya kwanza na yale yaliyofanywa na Mlawa.
Akarudi, wengine wanasema alitumia hila, kwa kuwa nafasi hiyo ilikuwa apewe Dk William Mgimwa. Pamoja na kurudishwa akashindwa zaidi na kupata anguko kubwa la kisiasa. Galinoma akawa katika wakati mgumu katika kipindi chake chote cha ubunge kati ya mwaka 2005 na 2010.
Kushindwa kwake kutekeleza ahadi mbalimbali alizoahidi kulimpa aibu, alikuwa akizomewa kwenye baadhi ya matukio ya kichama na kiserikali; akawa mnyonge katika siasa za jimbo hilo.
Mwaka 2010, Galinoma hakurudi tena, akaingia mitini, hakushiriki kura za maoni za chama chake CCM akihofia aibu kubwa:Januari 26, 2012 alifariki dunia.
Katika uchaguzi wa 2010, wananchi wa jimbo hilo wakakataa kumrudisha Mlawa pamoja na kurudi kwa nguvu kubwa kwenye harakati za kura za maoni za chama hicho; wakahisi litakuwa kosa kumrudisha kwasababu anaweza kuwa kama mtangulizi wake Galinoma na badala yake wakampa Dk William Mgimwa.
Dk Mgimwa akaingia kwa kasi kubwa, amefanya mengi akiwa mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Fedha; kifo chake kinaelezwa na wananchi wa jimbo hilo kuacha pengo kubwa wanaloamini linaweza kuzibwa na mwanae Godfrey Mgimwa.
Mgimwa anayo kazi kubwa ya kufanya ili yamsikute yaliyomkuta Galinoma na Mlawa. Kazi hiyo si nyingine, ni kazi ya kuziba pengo lililoachwa na marehemu baba yake na kutekeleza ahadi nyingine nyingi ambazo yeye mwenyewe amezitoa.
Ameapa; baada ya kuapa asitumie muda mwingi jijini Dar es Salaam, ni muhimu katika kipindi hiki kifupi akawa jirani na wapiga kura wake, vinginevyo atakuwa na mtihani mkubwa mbele yake.
↧
UNYAMA HUU HADI LINI? MWANAMKE AJIFUNGULIA KWENYE NDOO ATUPA KICHANGA CHOONI
MWANAMKE aliyejulikana kwa jina la Hadija Mohammed, mkazi wa Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam amekumbana na mkono wa sheria baada ya kufanya kitendo cha kinyama kufuatia kujifungulia kwenye ndoo kisha kichanga kukitupa chooni.
Kwa mujibu wa chanzo, mwanamke huyo alikuwa na ujauzito uliotimiza miezi tisa na kila mtu alikuwa akiuona, lakini ghafla siku ya tukio baadhi ya ndugu waligundua kuwa hakuwa na ujauzito tena!
NDUGU WAMBANA
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa baadhi ya ndugu na majirani walipomuona bila ujauzito walimbana kwa kumuuliza iliko mimba hiyo.“Ndugu zake na majirani walipomuona hana tumbo kama mwanzo walishangaa, wakaamua kumbana tena kwa vitisho kwamba watampeleka polisi.
“Ndipo alipoamua kueleza ukweli kwamba, alijifungulia kwenye ndoo lakini mtoto alikwenda kumtupa chooni,” kilisema chanzo hicho.
POLISI WAAMBIWA, WAKOMAA NAYE
Habari zilizidi kudai kuwa baada ya majirani na ndugu kuambiwa hivyo walikwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Pangani kilichopo Ilala, Dar ambapo walifika na kukiokoa kichanga hicho lakini walikuta kimeshakata roho.
MAMA APELEKWA POLISI
Mpashaji wetu alizidi kudai kuwa, baada ya polisi kuuchukua mwili wa mtoto huyo hawakumwacha mama mtu aendelee kuponda maisha uraiani, walimbeba mpaka kituoni hapo na kumfungulia jalada lenye namba ILA/RB/1715/2014 kisha kumpeleka kwenye Mahabusu ya Polisi Msimbazi huku mwili wa mtoto huyo ukipelekwa Hospitali ya Amana na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
NI FUNDISHO
Afande mmoja ambaye aliomba jina lake lisiandikwe, alisema ni lazima Hadija apambane na mkono wa sheria ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wenye mchezo huo.
“Hii tabia imekua sana. Wanawake wengi wanajifungua kisha wanawatupa watoto chooni au kokote kusikojulikana ili wao waendelee kula raha mjini. Huyu lazima sheria ishike makali yake ili iwe fundisho,” alisema afande huyo.
↧
MAZISHI YA KADA WA CHADEMA GERVAS KALOLO , IRINGA HAIJAPATA KUTOKEA
Wanahabari kutoka IMTV Sophin Mpunga kutoka kulia ,Ziada Mnyawami , Janeth Matondo ,Sima Bingileki na Prica
Waombolezaji |
Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard akichangia |
Msafara wa kuekea kuzika |
Msafara kuelekea kuzika |
Msafara kuelekea makaburini |
Baadhi ya wadau wakielekea kuzika |
Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi Chadema akiweka udongo |
Ndugu wakiweka mashada |
Ndugu wa kalolo kutoka Kenya akiweka shada |
Mstahiki meya Amani Mwamwindi akiweka shada la maua |
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza akiweka shada |
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiweka shada la maua katika kaburi la kada maarufu wa Chadema mkoa wa Iringa Gervas Kalolo wakati wa mazishi yaliyofanyika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa
...................................................................................................................................
MAZISHI ya kada maarufu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Gervas Kalolo yatikisa mji wa Iringa baada baada ya magari zaidi ya 100 na boda boda na bajaji zaidi ya 200 kupamba msafara wa mazishi hayo jana
Mazishi hayo ambayo yaliongozwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa yalionyesha kuvunja rekodi ya mazishi yaliyopata kufanyika katika mji wa Iringa .
Awali utaratibu wa mazishi hayo ulitaka kuvurugika kutokana na vijana wa Chadema kuanza kuzomea makaburini wakati Mc wa mazishi hayo wakati akitambulisha taratibu za watoa salam mbali mbali na kumtaka mwakilishi wa chama cha mapinduzi (CCM) huku akishindwa kumtaja mwakilishi wa Chadema na kuishia kusema kutakuwa na mwakilishi wa chama bila kutaja jina la chama husika .
Hata hivyo baada ya MC huyo kufuatwa na diwani wa Chadema kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi na kumlazimisha kutaja jina la Chadema badala ya kuishia kutaja chama bila jina lake ,ndipo alipolazimika kuepusha vurugu kwa kutaja jina la chama cha Chadema na kupelekea kuibuka kwa shangwe katika msiba huo.
Mbali ya kuibua shangwe kwa kuimba wimbo wa Chadema Chadema alisimama mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Msigwa ambae pia alishangiliwa kwa nyimbo hizo za Chadema .
Akizungumza katika mazishi hayo mbunge Msigwa mbali ya kumshukuru mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi na viongozi wa CCM kwa kushirikiana na chama katika mazishi hayo bado alisema kuwa kimsingi siasa katika msiba huwekwa kando.
Mbunge Msigwa alisema kuwa kiongozi yeyote na mtu yeyote mchango wake hupimwa kwa matendo yake na kuwa umati wa wananchi waliojitokeza katika mazishi hayo ni wazi kuwa Kalolo alikuwa ni kiongozi wa mfano katika jamii na kuwa Chadema itamuenzi kwa kusimamia msimamo wake wa kupinga ufisadi .
Kwa upande wake mwakilishi wa CCM katika mazishi hayo Shadrack Mkusa alisema kuwa Kalolo ambae alipata kuwa diwani wa kata ya Miyombini Kitanzini kabla ya kushindwa katika kura za maoni na kujiunga na Chadema.
Alisema kuwa Kalolo anakumbukwa kwa mengi ambao amepata kuyafanya likiwemo la kusimamia hoja zake katika vikao vya madiwani pamoja na kujitolea kusaidia watoto yatima katika kata yake.
↧
↧
SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII NSSF LATOA SEMINA KWA WACHIMBAJI WADOGO WAMADINI MWANZA.
↧
TANGAZO , NYUMBA YA KUUZWA INATAFUTWA MJINI IRINGA
↧
NYUMBA HII ILIYOKUWEPO ENEO LA ZIZI LA NG'OMBE MJINI IRINGA KWA SASA HAIUZWI IMEPATA MTEJA
NYUMBA HII INAUNYWA IPO ZIZI LA NG'OMBE IRINGA MJINI NI TSH MILIONI 14.5
Tunawaomba radhi wadau ambao mmeendelea kupiga simu kutaka nyumba hii iliyokuwepo eneo la Zizi la Ng'ombe mjini Iringa kwa sasa nyumba hii tayari imenunuliwa hivyo haiuzwi tena ,kwa yeyote anayehitaji nyumba kupanga kupangisha au kununua ama kuuza ,kiwanja ,shamba ama gari wasiliana nasi kwa namba hii 0754 026299↧
MIYEYUSHO VS MOHAMED MATUMLA WAPIMA UZITO KUPIGANA MAY 10 JUMAMOSI P.T.A SABASABA
Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakitunishiana msuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba siku ya jumamosi ya may 10 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Mohamed Matumla akipima uzito
↧
↧
BAADA YA UCHOVU WA KAZI::LEO NI AMSHA AMSHA NA SKYLIGHT BAND PALE THAI VILLAGE USIKOSEEEEEEE
Wanamwita Sam Mapenzi mzee wa Sauti nyororoooo akipagawisha vilivyooo ndani ya Thai village
Maua mazuriiiii ya Skylight band kutoka kushoto ni Aneth kushaba(AK 47) Digna mpera na Winfrida Richard wakiwa wanapata uphoto wenye ISO za kutoshaaa ndani ya Thai Village
Mpiga Drums wa Skylight band akiwa na furaha ya kutosha baada ya kuona mashabiki wake wanafurahia upigaji wake mahiri na wa kusisimua ndani ya Thai Village
Testimon Testimony ehhhhhh ni furaha yakutosha kwa mashabiki hawa wa Skylight Band wanayoipata kutoka kwa Bendi yao ya kijanja na iliyokamilika kila idara.
Mwanamuziki wa Skylight band Sam Masamba akiyarudi mangoma makali yaliyokuwa yakiporomoshwa naye na Wenzie,yani ni raha tupuuu ukiwa unapata ladha tamu za skylight band.
Aiiiiiii Aiiiiiii Aiiiii ni Aneth kushaba akiyarudi mauno mororoooooo kuwapagawisha mashabiki wake ndani ya Thai village
Mpenzi wangu nasema mi sikufanyaaaaaaaaaaaa,hapo aneth kushaba akiimba kibao matata cha kariakooo ndabi yaThai Village
Anaitwa Hashimu Donode akiimba kwa umakini na hisiaa kuwapagawisha wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village
Kutoka kushoto ni Winfrida Richard,Hashimu Donode na Digna mpera wakiwa mguu pandeeee sasa kuwapagawisha wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village
Wazeeee wa Jsb mpooooo tupooooooooo,wakiyarudi kwa utamuuuuu masebene yanayoporomoshwa kwenye kiota cha Thai Village na Bendi yao ya Skylight.
Mashabiki wa skyligth wakifurahia muziki mzuriiiii toka kwa bendi yao nzuriiiiii ya Skylight band ndani ya Thai Village.
Toka kushoto ni Joniko Flower,Aneth kushaba na mwenzao wakiyarudi mauno kwa umaridadi kabisaaaaaa kuwaburudisha mashabiki wao ndani ya Thai Village.
Gere mama gereeeeeeeee,ni mduara mkaliiiiii na mzuriiiiii ukiporomoshwa na bendi ya Skylight kwa mashabiki wao ndani yaThai Village.
Mratibu akinyoosha mikono juuuuu juuuuu akifeeeel hapyyyyy hapyyyyyyyy ndani ya Thai Village akiwa na mdau wa bendi na shabiki mkubwaaaa wa muziki mzuri wa Skylight Ban
↧
BASI LA DAR EXPRESS LAPATA AJALI ENEO LA WAMI
↧
WANA CCM TAWI LA CHUO KIKUU CHA MKWAWA WAWAONYA UKAWA KUACHA KUGEUZA BUNGE LA BAJETI KUWA BUNGE LA KATIBA ,WASEMA SERIKALI NI MBILI
Mwenyekiti wa tawi la chuo kikuu cha Mkwawa Thea Ntara (kushoto ) akiwapokea wageni |
Wanachama wa tawi la chuo kikuu cha Mkwawa |
Kaim katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kulia akiwa na viongozi mbali mbali |
Kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kulia akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa kada wake Wilison aliyejiunga na CCM |
Kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw Hassan Mtenga akimkabidhi kadi ya CCM kada wa Chadema Bw Wilison kushoto |
Kada wa Chadema aliyejiunga na CCM akivishwa skafu ya CCM |
Kada wa Chadema aliyejiunga na CCM akila kiapo na wenzake |
Mwanachama mpya wa UWT Mariam Mhewa akikabidhiwa kadi yake na katibu wa UWT Iringa mjini |
Kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akigonga cheazi na mwenyekiti wa CCM tawi la chuo kikuu cha Mkwawa Bi Thea Ntara |
Kada wa Chadema aliyekimbilia CCM Bw Wilison akigonga grasi na kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kulia |
Mwenyekiti wa CCM tawi la chuo kikuu cha Mkwawa Bi Thea Ntara akimpongeza Bw Wilison |
Makada wa CCM tawi la chuo cha Mkwawa wakiandaa msosi |
Makada wa CCM tawi la chuo kikuu cha Mkwawa wakiwa katika kikao jioni ya leo |
Wakizungumza leo wakati wa kikao cha kutathimini miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na kuwapongea wanachama wapya na wale waliotoka chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema )
Mwenyekiti wa tawi hilo la chuo kikuu cha Mkwawa Thea Ntara alisema kuwa wanashangazwa kuona bunge la bajeti limegeuzwa na sehemu ya bunge la katiba kwa wajumbe wa bunge la katiba ambao walisusa kikao kuchanganya mambo ndani ya bunge hilo.
Ntara alisema kuwa kimsingi mambo ya bunge la katiba yalipaswa kuzungumzwa ndani ya kikao husika ambacho UKAWA walitoka nje kwa kususa ila kwa sasa mambo ya bunge la katiba yasubiri muda wake na sio ndani ya bunge hilo la bajeti.
Wanachama hao ambao ni wanafunzi wa chuo hicho na wafanyakazi wa chuo hicho walisema kwa upande wao kama wasomi wanaona muundo wa serikali utakaowafaa watanzania ni serikali mbili na si zaidi ya hapo .
Alisema kuwa kinachopaswa kufanywa na wajumbe wote wa bunge la katiba kuangalia changamoto mbali mbali zilizopo katika muungano na kuzifanyia kazi badala ya kuuvunja muungano na kujikita kupigania muundo wa serikali tatu ambazo si mahitaji sahihi ya watanzania.
Hata hivyo alisema kuwa jumla ya wanachama wanaounda tawi hilo ni 306 wakiwemo watumishi 135 na wanafunzi ni 171
Hata hivyo alisema kuwa hatua ya serikali kuruhusu vyuo kuanzisha matawi ni sehemu ya kujipongeza kwa ukuaji mkubwa wa Demokrasia nchini.
Katika hatua nyingine Ntara aliwapongeza wanachama wapya 29 waliojiunga na tawi hilo akiwemo mmoja kutoka chama cha Chadema kuwa ni wazi wameona ndani ya upinzani hakuna jipya na badala yake ni chuki na fitna ndizo zinaendelea kuvitafuna vyama vya upinzani.
Akifungua kikao hicho mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Leticia Warioba mbali ya kuwapongeza wanafunzi na watumishi wa chuo hicho kwa kuanzisha tawi hilo bado alisema ni vema wanafunzi hao kuendelea kuelimisha wenzao juu ya umuhimu wa kutunza Amani iliyopo badala ya kuhamasisha uvunjifu wa Amani .
Kwa upande wake kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga aliwapongeza wanachama hao waliojiunga na CCM na jumuiya ya UWT na kuwataka kuendelea kuhamasisha wenzao kujiunga na CCM .
Aidha Mtenga aliwapongeza wasomi hao kwa kuanza kujiondoa Chadema na kurejea CCM na kuwa bado chama bora chenye mawazo ya kuwaletea maendeleo watanzania ni CCM na sio Chadema na vyama vingine ambavyo vimekuwa na utamaduni wa kususa mambo ya msingi bungeni.
↧
WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA AJALI YA MOTO MBEYA
“PRESS RELEASE”TAREHE 09.05.2014.
- WATOTO WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
- BIBI WA MIAKA 69 AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI.
- MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATOTO WAWILI WALIOTAMBULIWA KWA MAJINA YA 1. BARAKA LACKSON (04) NA 2. ESTER LACKSON (02) NA MIEZI 10 WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI BAADA YA NYUMBA WALIMOKUWA WAKIISHI KUUNGUA MOTO.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.05.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO KATIKA MTAA WA MAGEUZI MJI MKONGWE, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA UTENGULE USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI , MKOA WA MBEYA. AIDHA MTOTO MARTIN KABWILILE (09) ALIJERUHIWA KWA KUUNGUA MOTO MIGUUNI NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO NI MSHUMAA ULIOKUWA UMEWASHWA NA WAHANGA CHUMBANI NA WAO KULALA.
MOTO ULIZIMWA NA WANANCHI KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA IFISI. WAKATI WA TUKIO WAZAZI HAWAKUWEPO NYUMBANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO NA KUCHUKUA TAHADHARI KUTOKANA NA MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. AIDHA NI VYEMA KUACHA MTU WA KUWAANGALIA WATOTO PINDI WANAPOKWENDA KATIKA SHUGHULI ZAO NA KUHAKIKISHA VITU KAMA MISHUMAA, VIBATARI NA MAFUTA YA DIESEL NA PETROL VINAWEKWA MBALI NA WATOTO KWANI NI HATARI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
BIBI WA MIAKA 69 MKAZI WA KATABE WILAYA YA RUNGWE AITWAYE AIDA MWANGOSIM AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI NA USONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA NYUMBANI KWAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KATABE, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. AIDHA KATIKA TUKIO HILO HAWA GEORGE (12) MWANAFUNZI SHULE YA MSINGI KATABE DARASA LA PILI AMBAYE NI MJUKUU WA MAREHEMU ALIJERUHIWA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI KISHA KUBAKWA NA AMELAZWA HOSPITALI YA MAKANDANA-TUKUYU.
CHANZO CHA TUKIO KINACHUNGUZWA, NDANI YA NYUMBA YA MAREHEMU KUMEKUTWA SHOKA NA JIWE MOJA KUBWA AMBAVYO VINADHANIWA KUTUMIKA KATIKA TUKIO HILO. UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOWAACHA WAJANE/WAZEE WENYE UMRI MKUBWA NA WATOTO WADOGO BILA UANGALIZI WA KARIBU ILI KUEPUSHA WATU WENYE NIA MBAYA/WAHALIFU KUTOPATA NAFASI YA KUTEKELEZA UHALIFU WAO. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE/WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI JANGURUTU DARASA LA TANO ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HABIBU DISMASS (11) AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.120 AMV AINA YA CAMRY LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DERAVA OTINO MWAMPAMBA (48) MWALIMU SHULE YA SEKONDARI, MBARALI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.05.2014 MAJIRA YA SAA 16:15 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MABANDA, KATA NA TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVAAMEKAMATWA NA GARI LIPO POLISI-RUJEWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA PEMBENI MWA BARABARA NA KUVUKA SEHEMU ZENYE VIVUKO ILI KUEPUKA AJALI.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
↧
↧
IGP AFUNGUA MAFUNZO YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA



↧
KINANA AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA MTO MBUTU
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mhandisi Makoye Luhya wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la mto Mbutu ambalo litasaidia zaidi ya watu 130,000 .Daraja hilo pia litasaidia sana wakulima wa pamba na nikiunganishi cha Tabora na Shinyanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua Daraja la Mbutu wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akisaidiana na wajenzi wa Daraja la Mbutu wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
![]()
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kutoka juu ya daraja la Mto Mbutu baada ya kulikagua na kuona maendeleo ya ujenzi wa daraja.Katibu Mkuu wa CCM yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoani Tabora.(picha na Adam Mzee)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua Daraja la Mbutu wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akisaidiana na wajenzi wa Daraja la Mbutu wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kutoka juu ya daraja la Mto Mbutu baada ya kulikagua na kuona maendeleo ya ujenzi wa daraja.Katibu Mkuu wa CCM yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoani Tabora.(picha na Adam Mzee)
↧
VIDEO YA NAPE AKIZUNGUMZIA KILIO CHA WAKULIMA WA PAMBA IGUNGA
↧