↧
BREAKING NEWS:MSIBA MKUBWA LUDEWA
↧
MAZISHI YA BABA MAZAZI WA MBUNGE FILIKUNJOMBE KUFANYIKA SIKU YA JUMANNE LUDEWA MJINI ,VIONGOZI MBALI MBALI WAKIONGOZWA NA RAIS KIKWETE WATUMA SALAM ZA RAMBI RAMBI
Mzee Filikunjombe kushoto akiwa katika moja kati ya ibada na waumini wengine |
Mzee Filikunjombe wa pili kushoto akiwa na mzee Kihaule ambae pia ni marehemu na Mbunge Simalenga wakimsimika Deo Filikunjombe baada ya kutangaza nia ya kuwania ubunge Ludewa mwaka 2010 |
![]() |
Waziri mkuu Mizengo Pinda kushoto akizungumza na mzee Filikunjombe ambae sasa ni marehemu enzi za uhai wake |
↧
↧
TANROADS SHINYANGA LAWAMANI
Na Wiliam Bundala matukiodaima.com kanda ya Ziwa
Wakala wa barabara Tanzania TANROADS mkoani Shinyanga imelalamikiwa na wananchi wa kata ya Igunda wilayani Kahama kwa kushindwa kusimamia vyema ujenzi wa barabara ya kutoka nyandekwa – butibu hali ambayo hivi sasa imezolewa na maji licha ya kujengwa mwaka huu katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Malalamiko hayo yaliwasiliswa jana mjini kahama na Diwani wa kata ya Igunda Tabu Katoto ambaye amesema hivi sasa barabara hilo katika kijiji cha Kakebe limekatika kabisa na hakuna mawasiliano ya pande mbili za nyandekwa na Igunda.
Katika malalamiko hayo Katoto amesema licha wananchi kulalamikia ujenzi hafifu uliokuwa ukifanywa kwenye barabara hiyo lakini meneja wa TANROADS mkoa wa Shinyanga alikuwa Hafuatilii licha ya wananchi hao kumpelekea taarifa.
Kwa upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Shinyanga Augustino Filipo alipohojiwa kwa njia ya simu na Redio Free Afrika amesema swala hilo la kukatika kwa barabara hiyo analifahamu na alikwisha mweleza diwani huyo kwa kumfafanulia zaidi.
Filipo amesema fedha zilizo kuwa zimetengwa ni kwajili ya kilometa 14 kutoka Kahama mjini kwenda Nyandekwa ambapo barabara hiyo imejengwa kwa kiwango cha juu na kutoka hapo hadi Igunda kupitia Kakebe panapolalamikiwa hakukuwa na fedha za kutosha kujenga kwa kiwango cha juu.
Amesema eneo lililozolewa na maji lilijengwa kwa kiwango cha chini kuling ana na fedha kidogo zilizokuwepo hali iliyosababisha kupishana ubora na ile barabara ya kilometa 14 iliyojengwa kwa kiwango cha juu ambayo Diwani huyo anataka ubora uwe sawa na ile iliyojengwa kwa kiwango cha chini kutokana na ufinye wa bajeti yake.
↧
AFRICAN BARRICK YAANZA KASI YA MALIPO YA MRAHABA KWA HALMASHAURI YA USHETU NA MSALALA....YATOA BILIONI MOJA NA MILIONI MIATATU
Na William Bundala(Kijukuu)
Matukio Daima Kanda ya ziwa.
Kampuni ya Afrikan Barrick Gold Mine LTD kupitia mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu wilayani Kahama imetoa kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni miatatu katika halmashauri mbili za Ushetu na Msalala.
Hali hiyo imebainishwa jana na mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Juma Kimisha katika kikao cha baraza la Madiwani ambapo amedai fedha hizo ni mrahaba wa malipo ya miaka minne katika Halmashauri ya wilaya ya Kahama kabla ya kugawanywa kuwa Ushetu na Msalala.
Katika kikao hicho Kimisha amesema fedha hizo Halmashauri yake ya Ushetu imepata milioni 610 huku zilizobaki zimebaki katika halmashauri ya Msalala ambako ndipo mgodi huo wa Bulyanhulu ndiko unakofanyia shughuli zake za uchimbaji dhahabu.
Aidha katika baraza hilo Kimisha amewaambia Madiwani fedha hizo shilingi milioni 450 zitumike katika maendeleo mengine ikiwemo umaliziaji wa majengo ya zahanati nyumba za walimu vyumba vya madarasa na maabara katika shule za Sekondari za kata.
Kabla ya hapo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Egdius Kahendaguza amewaambia Madiwani hao katika fedha hizo milioni 147 zitumike kununulia gari ili kupunguza matatizo ya ukosefu wa usafiri kwa wataalamu wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
Halmashauri hiyo ya Ushetu ni moja kati ya Halmashauri zingine mbili za mji na Msalala zinazounda wilaya ya Kahama lakini Kijografia yake shughuli zake zote ziko nje ya mji wa Kahama kuanzia km 30 hadi 40 kutoka mjini zilipo ofisi zake ili kuwafikia wananchi wake lazima kusafiri umbali huo huku ikikabiliwa na upungufu wa magari.
↧
FLASHBACK VIDEOS,MWIGULU NCHEMBA ALIPOTIKISA BUNGE MARA TATU KWA NYAKATI TOFAUTI
Kutokana na Kukua kwa Kasi Kisiasa kwa Mwanasiasa Kinda Mh:Mwigulu Nchemba hapa Nchini kupitia Chama cha Mapinduzi,Licha ya Kuwa Mwanasiasa anayevuta tension kwa Mwananchi yeyeote anaposikia anazungumza ama Bungeni au sehemu yoyote ile Jukwaani au Kwenye Vyombo vya Habari kwa namna anavyojenga hoja zake kwa Mlengo wa Utaifa,Maslahi kwa Wananchi na Uzalendo wa hali ya Juu,Hii leo nimeguswa angalau Kukupa nafasi ya Kuangalia angalau Video tatu ambazo Katika Michango yake ndani ya Bunge Zimekuwa Gumzo sana.
Video Na.1"Achanachana Bajeti ya Upinzani Bungeni"
Hii ni Video ambayo Mh:Mwigulu Nchemba aliweka Historia kwa Mara ya kwanza ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akichangia Bajeti ya Nchi Mwaka 2012/2013.Hii Video inatajwa kuwa ndio Iliweka Gumzo kwa Wanasiasa Nchini hasa Upinzani.Inasemekana Upinzani walianza hapa Kutambua Moto wa Mwigulu Nchemba kwenye Siasa.VIDEO 2:
"Ahojia Uandishi wa Tarakimu kwenye Bajeti ya Upinzani"
Kwenye Video hii Mh:Mwigulu Nchemba anahoji Mapungufu Makubwa ya Uandishi wa tarakimu kwenye Bajeti ya Upinzani,Hususani Kushinda kuandika Bilioni kwa tarakimu.
VIDEO: 3.
"Akichangia Bunge la Katiba 2014.Ahoji Mbowe na Jusa Kutaka Kupitisha Swala la Ushoga KimyaKimya"?.
Kwa mara ya kwanza akichangia Kweneye Bunge Maalumu la Katiba Mwaka 2014,Mh:Mwigulu Nchemba aamua kuweka wazi kuwa Kufanya mambo kwa Siri kuna watu wanataka Kupitisha Mambo Mabaya kwa Taifa Kimya kimya likiwamo Ushoga.>Angalia Video.
Video Zipo Nyingi alizochangia Bungeni,Lakini hizi ni baadhi tu zilizotikisa Nchini na Uga wa Siasa.
Na Mdau Wetu Mtanzania Mzalendo.
Na Mdau Wetu Mtanzania Mzalendo.
↧
↧
WANAHABARI IRINGA WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA
Wanahabari mkoa wa Iringa wakiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari kwa kufanya usafi |
Hapa wakiendelea kuzoa takataka |
Wananchi waliounga mkono jitihada hizo |
↧
DACICO F.C YAIGARAGAZA MLIMANI PROFESIONAL
Na: Recho George/Edger Kaizer, DACICO COLLEGE.
Timu ya Mpira wa Miguu ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala, Dar es Salaam City College,(DACICOFC),hatimaye imefanikiwa kuifunga Timu ya Mlimani Profesional F.c kwa 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika majira ya jioni katika uwanja wa Bwaloni uliopo mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam Jana. Katika mchezo huo ambao mashabiki wa timu ya Dacico F.c walionekana kutoa shutuma nyingi kwa Mwamuzi kutokana na kitendo chake cha kutowasikiliza mashabiki wakati mchezo ukiendelea kwa kile walichodai kuwa alikuwa akionyesha upendeleo kwa wapinzani wao timu ya Mlimani F.c.
Akizungumzia mchezo huo kocha wa timu ya Dacico fc Moris Chambua alisema kuwa “Kiwango cha Mpira kilichoonyeshwa na Kikosi cha wachezaji wangu ndiyo silaha iliyowafanya wakaibuka na ushindi huo”alisema kocha huyo.
Na Kwa upande wa kocha wa timu ya Mlimani Professional yeye alisema kuwa” timu yake ilicheza vizuri lakini walizidiwa mbinu chache za kiufundi hali iliyopelekea timu yake kupoteza mchezo huo”alisema Fredrick Emanuel.
Wakati mashabiki wa timu hizo walisema kuwa “timu ya dacico ilikuwa na uwezo wa kushinda zaidi ya goli moja walilolipata lakini washambuliaji wa timu hiyo hawakuwa makini kwenye suala zima la umaliziaji” alisema Fack A. Fack shabiki wa Dacico F.c, na kwa upande wa shabiki wa mlimani professional Mohamed hawadh yeye alisema kuwa “uwanja umechangia wao kutofanya vizui kutokana na uwanja huo kujaa tope” alisema mohamed
Mchezo huo ambao ulianza saa kumi na dakika arobaini jioni kutokana na hali ya hewa ambayo kwa wakati mwingi Mvua za hapa na pale( Rasharasha) zilisababisha kucheleweshwa kwa Mtanange huo ambao hata hivyo pamoja na Mvua Mashabiki waliendelea na shamrashamra zao hadi mwisho wa mchezo.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika katika mpambano huo, timu zote zilikwenda mapumziko mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa kutofungana kutokana na wachezaji wa pande zote mbili kucheza kwa kukamiana wakati wote pamoja na washambuliaji wa pande zote kutokuwa makini wakati wa umaliziaji.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo kwa upande wa timu ya Dacico, kocha wa timu hiyo Moris Chambua aliwatoa Mohamed Abdalah na nafasi yake ikachukuliwa na mchezaji Razack Mushi, alitoka Alafa Julius(a.k.a Mbaba) na nafasi yake kuchukuliwa na Jafet Mantari, alitoka Moody Mohamed na nafasi yake kuchuliwa na Sixmond wakati Mlimani wao waliwaingiza Mrisho Mrisho na Baraka S. Baraka mabadiliko ambayo yalionekana kuipa nguvu timu hiyo.
Baada ya Makocha wa timu zote mbili kufanya mabadiliko hali ya mchezo ilibadilikia pia kutokana na kuingia wachezaji wenye nguvu ambapo kwenye dakika ya 58, 66, 70 mwamuzi wa mpambano huo, Shaaban Mpalule ambaye ni Mwalimu katika chuo cha Dar es Salaam City College, alipuliza filimbi mara kwa mara wakati wachezaji wa Timu ya DACICO walipokuwa wakielekea kufunga kuwa Wameotea.
Kipindi cha pili katika dakika 64 hadi 72 timu ya Mlimani Profesional ilionekana kuelemewa zaidi na Wenzao wa DACICO F.c kabla ya dakika 73 hadi 81 ambapo Mlimani baada ya kufanya mabadiliko, ilionekana kupata nguvu na kuanza kulishambulia lango la timu ya Dacico lakini bahati haikuwa upande wao kutokana na Dacico kupata Penalti katika dakika ya 82 ya mchezo na iliweza kuwekwa kimiani na kiungo mchezeshaji Jafeti George, ambaye alifunga kwa Shuti kali lililokwenda moja kwa moja kimiani na kumshinda mlinda mlango wa Mliman Briy B. Briy.
Baada ya mchezo kumalizika mwandaaji wa mpambano Alexander Ngerezi alisema kuwa maandalizi ya mchezo yalikwenda vizuri isipokuwa kulikuwa na mapungufu madogo madogo ambayo yalihitaji msaada wa wadhamini ikiwamo masuala ya mipira, jezi, Filimbi, pamoja na Viatu kwa Wachezaji ambao muda mwingi wanatumia kuwa masomoni hivyo kukosa muda wa kufuatilia vifaa vya michezo, katika mpambano wa kwanza pia timu ya Dacico iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala cha Dar es Salaam City College(DACICO TANZANIA) uliopo Kibamba Chama jijini Dar es Salaam.
↧
BONDIA MYWEATHER AMSHINDA KWA POINT MAIDANA ,MATUMLA,CHEKA, KALAMA WAANGALIA LIVE IGO LOUNGE SINZA DAR
![]() |
Bondia Floyd Myweathe kushoto akipangua ngumi ya Marcos Maidana wakati wa mpambano wao uliochezwa alfajili ya kuamkia leo point za majaji, Judge Michael Pernick scored it 114-114, a draw. Bert Clements had it 117-111 and Dave Moretti score it 116-112 |
![]() |
Bondia Floyd Myweather kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Marcos Maidana wakati wa mpambano wao uliochezwa alfajili ya kuamkia leo point za majaji, Judge Michael Pernick scored it 114-114, a draw. Bert Clements had it 117-111 and Dave Moretti score it 116-112 |
Mabondia wa Tanzania Kalama Nyilawila kushoto,Rashidi Matumla na Fransic Cheka wakifatilia kwa makini mpambano huo uliochezwa alfajili ya leo katika ukumbi wa Igo Lounge sinza mapambano walipokuwa wakionesha live kupitia luninga kubwa kwa mashabiki wa mchezo huo |
TANGAZO LIKIONESSHA KUWEPO KWA NGUMI ZA LIVE KUPITIA LUNINGA
Mabondia Rashid Matumla kushoto,Fransic Cheka na Kalama Nyilawila wakifatilia mpambano wa Myweather na Maidana kupitia luninga katika ukumbi wa Igo lounge sinza mapambano
makamu wa rais Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT)? Anderson Lukelo, mabondia Rashid Matumla kushoto,Fransic Cheka na Kalama Nyilawila wakifatilia mpambano wa Myweather na Maidana kupitia luninga katika ukumbi wa Igo lounge sinza mapambano leo wakiwa na wadau mbalimbali wa masumbwi nchini
mashabiki wakifurahia mchezo wa ngumi kupitia luninga
MYWEATHE NA MAIDANA WAKIPAMBANA LIVE KATIKA LUNINGA
Bondia Fransic Cheka akitoa tasmini ya mchezo ulivyokuwa baada ya myweathe kutangazwa mshindi
Bondia Kalama Nyilawila akitoa tasmini ya mchezo ulivyokuwa baada ya myweathe kutangazwa mshindi
wadau mbalimbali wakipiga picha na cheka picha na www.superdboxingcoach.blogspot.comNa Mwandishi Wetu
MABONDIA mbalimbali alfajili ya kuamkia leo wamejitokeza kuangalia mpambano uliokuwa ukifanyika Marekani kati ya bondia Floyd Myweather na Marcos Maidana mpambano uliokuwa unafanyika katika ukumbi mkubwa kabisa wa ngumi duniani MGM grand
ambapo hapa nchini mabondia Rashidi Matumla, Kalama Nyilawila pamoja na Fransic Cheka na makamu wa rais Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT)? Anderson Lukelo pamoja na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
walijumuika kwa pamoja kuangalia mpambano huo live katika ukumbi wa
Igo lounge uliopo sinza mapambano
mpambano huo ulikuwa mkali ambao dunia nzima ya wapenda mchezo wa ngumi walikuwa wakisubili kwa hamu kuangalia wakali hawo wa masumbwi wanavyo oneshana umwamba
hata hivyo mpaka dakika ya mwisho ya mpambano huo ulisha kwa bondia Floyd Myweather kushinda kwa pointi za majaji wawili na mmoja wa majaji akitoa droo mpambano huo
Michael Pernick scored, 114-114, a draw. Bert Clements , 117-111 and Dave Moretti , 116-112
Michael Pernick scored, 114-114, a draw. Bert Clements , 117-111 and Dave Moretti , 116-112
wakizungumzia mpambano huo walio uona live kupitia luninga bondia Rashid Matumla alisema wenzetu wana uwezo mkubwa sana katika masumbwi ata katika kujaji maidana alikuwa anacheza fujo tu katika mchezo huu hivyo ndio kitu kilicho mnyima ushindi
nae cheka aliongeza kwa kusema siku zote bingwa analindwa sana hivyo myweather ameweza kutetea taji lake vizuri
nae kalama amesema mambo haya yanatokea kila siku mana nakumbuka zama za Tyson ndio watu walikuwa wanajazana namna hii kuamka alfajili kuangalia ngumi sasa myweather anatisha kachukua urithi wa Tyson huyu bondia ni mzuri kwa jkutembea awapo ulingoni kacheza vizuri nimemfurahia
↧
VIDEO CLIP YA NAPE NNAUYE ALIPOHUTUBIA GOMBANI YA KALE PEMBA
↧
↧
TANZANIA INA UPUNGUFU WA MADAWATI MILIONI 1.4 - PINDA
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema shule za msingi hapa nchini zinakabiliwa na upungufu wa madawati karibu milioni moja na nusu ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ijifunge mkanda na kulipa kipaumbele suala la kupunguza tatizo hilo.
Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Mei 3, 2014) wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ambao walihudhuria uzinduzi wa Wiki ya Elimu Tanzania kwenye uwanja wa Jamhuri.
“Takwimu nilizonazo zinaonyesha kuwa Tanzania ina mahitaji ya madawati 3,302,678 wakati madawati yaliyopo ni 1,837,783 kwa hiyo tuna upungufu wa madawati 1,464,895 katika shule zetu za msingi,” alisema Waziri Mkuu.
Kutokana na mahitaji hayo, Waziri Mkuu alisema endapo Serikali itaamua kutengeneza madawati 100,000 kwa mwaka kwa gharama ya sh. bilioni 12/-, itachukua miaka 15 kumaliza tatizo hilo ili kuziba pengo lililopo sasa.
“Nimepita kwenye banda la Taasisi ya Maajar Trustna pale wameniambia kuwa wameshatengeneza madawati 12,000 na kuyagawa katika mikoa sita. Wastani wa kila dawati ni sh. 120,000/- lakini inategemea na upatikanaji wa mbao pamoja na gharama za ufundi.”
“Tukichukua gharama zao, tukaamua kutengeneza madawati 200,000 kwa mwaka, itatugharimu sh. bilioni 24 na itachukua miaka saba kumaliza tatizo hilo wakati tukiamua kutengeneza madawati 300,000 kwa mwaka, itatugharimu sh. bilioni 36 na itachukua miaka mitano kumaliza tatizo hilo,” alifafanua Waziri Mkuu.
Alisema ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe kumaliza tatizo hilo kwani inatia aibu na hakuna sababu ya kuendelea kuona wanafunzi wakisoma huku wamekaa chini.
“Waziri wa Elimu na watu wako ni lazima mjifunge mkanda na kipaumbele chenu kiwe ni kupunguza tatizo la madawati katika muda mfupi sana; na itakuwa vema kama mtajipanga haraka ili mje na suluhisho ndani ya wiki hii kabla Mheshimiwa Rais hajaja kufunga maonyesho haya,” aliongeza.
"Kaeni na watu wa Taasisi ya Maajar Trustmuone ni kwa njia gani mnaweza kutatua tatizo hili… kama ni kuandaa chakula cha hisani ili kuchangia madawati fanyeni hivyo ili tatizo hili liishe. Wako Watanzania wanaweza kuchangia dawati moja, mawili, matatu au zaidi na tukajikuta tumemaliza tatizo hili,” alisema.
“Na ninyi wa TAMISEMI kaeni na kuandaa utaratibu wa kuondoa tatizo hili. Kila Halmashauri kwa nafasi yake iwe ya mjini au ya vijijini ina uwezo wa kupunguza tatizo kulingana na fursa ilizonazo. Nasisitiza jambo hili liwe ni ajenda ya kudumu,” aliongeza.
Wakati huohuo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idris Kikula, akitoa shukrani kwa niaba ya wadau wa elimu alisema anaunga mkono hoja ya uchangiaji wa madawati na kusisitiza kuwa kuna haja ya watu kubadili mtazamo walionao kuhusu suala la uchangiaji wa huduma za kijamii.
“Kuna watu ukiwaambia kuchangia madawati wanakataa lakini wako waliopokea kadi nyingi za michango ya harusi na wako tayari kuzichangia kwa sababu wanajua huko kuna kula na kunywa. Niwasihi wananchi tubadilishe mtazamo wetu na tuisaidie Serikali katika suala hili la madawati kwa watoto wetu,” alisema.
(mwisho)
↧
WAANDISHI WA HABARI MSIKUBALI KUTUMIWA, UNGANENI
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wakifanya usajili kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.(Picha na Zainul Mzige).
Na Waandishi Wetu, Arusha
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari na kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.
Kibanda aliyasema hayo jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuongeza kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti zao na kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.
“Baadhi ya wahariri huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari na kuyapa uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa hayawahusu moja kwa moja,” alisema Kibanda.
Aliongeza kwa kusema kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa vidole na kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama kuvitetea kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii.
Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.
“Kwa sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.
Kibanda aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha tatizo kwa kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.
“Kuwe na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kasongo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw. James Jesse, akitoa mada kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya uhuru wa kujieleza kwa kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yanayofikia kilele leo jijini Arusha.
Mwanahabari mwingine mkongwe Dokta Samwilu Mwaffisi aliyetoa mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari alisema kuwa kuna haja ya waandishi kuzingatia uhuru wa habari walionao kwa kuzingatia maadili yanayowaongoza ili kuboresha heshima waliyonayo katika jamii kwa kuandika ukweli na uhakika, bila upendeleo, kutoa fursa ya kujitetea na kukubali kuomba radhi pale unapokosea.
“Kuandika habari zenye kuzingatia maadili kunapunguza manung’uniko, mashauri na kuongeza heshima ya chombo cha habari na mwanahabari mwenyewe,”
Akizungumzia suala la ufanisi, Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari, Kenneth Simbaya, aliwaasa waandishi wa habari kusimamia ukweli katika kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo litakawaweka huru zaidi katika utekelezaji wa shughuli zao za uandishi wa habari.
Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na umoja wa asasi mbalimbali chini ya uenyekiti wa MISA TANZANIA unafikia kilele chake tarehe 3 Mei kwa kuzindua majarida mbalimbali, matamko kutoka asasi mbalimbali na kuhitimishwa kwa tafrija ya chakula cha jioni chini ya mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mheshimiwa Mark Bomani.
Mwanahabari Mkongwe kutoka Chuo Kikuu Huria, Dokta Samwilu Mwaffisi (kulia) akiwasilisha mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Simon Berege.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akitoa maoni yake wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakongwe, mabalozi na wanahabari washiriki katika kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Mwandishi wa Habari Chokonozi, Bw. Fredrick Katulanda, akielezea madhila mbalimbali yaliyomsibu katika utekelezaji wake wa kuandika habari za uchambuzi.
Mwanahabari Mkongwe Bi. Leila Sheikh akichangia mada ya Mchango wa Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Katika Utawala Bora, Kukuza Uwezo Na Kupunguza Umaskini wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Mmiliki wa Gazeti tando la Mjengwa na Kituo cha Redio Kwanza Jamii, Bw. Maggid Mjengwa akielezea jinsi Intaneti inavyoweza kuunganisha mtandao wa Redio.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) na Mkurugenzi wa kituo cha mawasiliano Sengerema, Bw. Felician Ncheye akichangia mada.
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamamo hilo.
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Picha juu na chini Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 likiendelea.
Mwanakamati wa maandilizi ya maadhimisho ya Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda nje ya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
↧
WASICHANA 30 JIJINI MWANZA WAPATIWA MAFUNZO YA SIKU TANO KUHUSU ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA MAJUMBANI.
Mkurugenzi wa shirika la kutetea Haki za Wanawake na Wasichana KIVULINI lenye makao yake makuu jijini Mwanza Bw. Ramadhan Masele amefunga rasmi mafunzo ya siku tano yanayolenga kuwajengea wasichana uwezo wa kutoa elimu juu ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia chini ya mradi wa kuwashirikisha vijana kuzui Ukatili wa majumbani ikiwa ni pamoja na ukatili wa kingono kwa watoto wa kike na wasichana.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo Bw. Masele aliwataka washiriki wote kutumia elimu hiyo muhimu waliyoipata kutoa elimu na kuongeza uwelewa zaidi kwa jamii yao kuanzia ngazi ya familia, marafiki na vikundi mbalimbali na kuwa chachu ya mabadiliko juu ya kupigania haki za wanawake na wasichana wanaonyanyaswa kijinsia katika jamii zao.
“Imani yangu ni kuwa semina hii itakuwa ni kiwanda kizuri cha kuwatengeneza nyinyi wote kuwa mabalozi wazuri katika jamii, baada ya mafunzo haya tunaamini kuwa mtakuwa chachu ya mabadiliko katika kutetea na kulinda haki za wanawake na wasichana kwa kukemea, Kupinga, kuripoti na kuzuia aina zote za ukatili wa majumbani na kingono kwa wasichana na wanawake na kutoa taarifa pindi vitendo hivi vinapotokea” alisema Bw. Masele
“Kila mmoja aliyehudhuria mafunzo haya kwa nafasi aliyonayo tunaamini anaweza kuwa chachu ya mabadiliko endapo atatimiza wajibu wake kwenye eneo analoishi. Hili suala la ukatili wa kijinsia si suala geni nchini hasa eneo hili la kanda ya ziwa hivyo kuna kila sababu ya kuzidisha mapambano dhidi yake, cha muhimu ni kuzingatia mafunzo mliyopewa na muwezeshaji wenu” aliongeza Bw. Masele.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku 5 kwa vijana 30 wa kike wenye umri kati ya miaka 18-24 kutoka wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela jijini Mwanza. Lengo la Mafunzo ni kuwajengea vijana uwezo wao binafsi na uwezo wa kuelimisha jamii hasa Vijana wenzao kupambana na kupinga Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana katika maeneo wanayoishi.
Mafunzo yalianza Jumatatu tarehe 28 Aprili, 2014 mpaka tarehe 2 Aprili, 2014 katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi, VETA kilichopo Nyakato nje kidogo ya jiji la Mwanza.
Takwimu zinaonyesha bado jamii inakabiliwa na ukatili mkubwa wa kijinsia ambapo ubeberu wa wanaume pamoja na mila na desturi potofu zimeonekana kukandamiza jinsi ya kike zaidi kuliko jinsi ya kiume, ukatili huo ni wa kijamii, kiuchumi pamoja na kisaikolojia hivyo kunaitajika juhudi za dhati na makusudi kuweza kukabiliana na tatizo lilopo kwa jamii.
Akimalizia mawaidha yake kwa washiriki Bw. Masele alisema lengo la mafunzo hayo ni kuona mabadiliko katika mfumo juu ya kujali na kuheshimu haki za mwanamke na wasichana, kwani jamii nyingi zinapambana na mifumo miwili mikubwa, ambayo ni mfumo dume ambao umekuwa ukiwakandamiza wanawake katika jamii na mfumo wa kitabaka unaoongeza nafasi kati ya matajiri na masikini.
Shirika la KIVULINI kwa kushirikiana na Asasi ya Vijana inayojulikana kama Wadada Centre for Solution Focus Approach ndio waandaji wa mafunzo hayo kupitia mradi wa kuwashirikisha vijana kuzui Ukatili majumbani na Ukatili wa Kingono chini ya ufadhili wa Shirika la terre des hommes ch (tdhschweiz) - Fursa kwa Vijana la nchini Switzerland
Kivulini ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kutetea pamoja na kulinda Haki za Wanawake na Wasichana. Shiriki la Kivulini linahamasisha jamii (Wanawake, Wanaume na Vijana ) kulinda, kutetea Haki za Wanawake na Wasichana kwa kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Makao makuu ya shirika yapo jijini Mwanza, Wilaya ya Ilemela, Tanzania.
↧
HATIMAYE MARKIA NA RAIS MPYA WA KIJIJI CHA MAISHA PLUS WAPATIKANA
Markia Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Elizabeth Masha kutoka Morogoro Tanzania
Rais Mpya wa Kijiji cha Maisha Plus Mary Masha kutoka Nchini Kenya
Ndani ya Kijiji cha Maisha Plus/ Mama Shujaa wa chakula kila siku ya Alhamisi huwa panafanyika uchaguzi wa kumpata Rais mpya ambaye anachaguliwa na Washiriki wenyewe wa Kijiji cha Maisha Plus ambapo kati ya hao mmoja hupatikana na Marais waliopita hawapatiwi nafasi ya kugombea tena, na kwamba mama yake na Rais huteuliwa moja kwa moja kuwa Markia wa Kijiji hicho.
Kazi ya uchaguzi ilianza Kijijini hapo ambapoidadi ya washiriki 36 wakiwemo vijana 16 na kinamama 20 Kila siku ya Alhamisi ni siku ya uchaguzi wa Rais wa kijiji cha Maisha Plus ambaye husimamia shughuli zote zinazofanyika katika kijji hicho.
Wiki hii washiriki 10 waliteuliwa kugombea nafasi ya urais ambapo 7 ndiyo waliopigiwa kura ya siri na kupata mshindi. Washiriki wawili kati yao hawakuweza kugombea nafasi ya hiyo kutokana na utaratibu uliopo kwamba aliyewahi kushika wadhifa huo kwa muhula uliopita hataweza kugombea tena.
Marais hao wa mihula uliyopita ni Bonifas Mang’anyi na Bakari Khalid wote watanzania. Abdul Karim kutoka Burundi alijitoa kwa kuwa hakuwa tayari kushika wadhifa huo kwa sasa.
Kwa kawaida kila kijana huwa na mama katika kijiji cha Maisha Plus na endapo kijana atachaguliwa kuwa Rais mama yake huwa Malkia ambaye humshauri Rais na kufanya maamuzi katika kijiji hicho.
Wiki hii washiriki 10 waliteuliwa kugombea nafasi ya urais ambapo 7 ndiyo waliopigiwa kura ya siri na kupata mshindi. Washiriki wawili kati yao hawakuweza kugombea nafasi ya hiyo kutokana na utaratibu uliopo kwamba aliyewahi kushika wadhifa huo kwa muhula uliopita hataweza kugombea tena.
Marais hao wa mihula uliyopita ni Bonifas Mang’anyi na Bakari Khalid wote watanzania. Abdul Karim kutoka Burundi alijitoa kwa kuwa hakuwa tayari kushika wadhifa huo kwa sasa.
Kwa kawaida kila kijana huwa na mama katika kijiji cha Maisha Plus na endapo kijana atachaguliwa kuwa Rais mama yake huwa Malkia ambaye humshauri Rais na kufanya maamuzi katika kijiji hicho.
Uchaguzi ulifanyika kwa wagombea 7 akiwemo Shida Mganga, Seif Mohamed, Ally Thabiti, Mbonimpaye Nkoronko na Hyasinta Hokororo kutoka Tanzania, Ngabozinza Daniel kutoka Rwanda na Mary Masha kutoka Kenya. Uchaguzi wa Rais ulifanyika mara mbili kwa kuwa washindi walipata kura sawa iliyopelekea kurudia kupiga kura ili kupata mshindi mmoja.
Washindi waliopata kura sawa ni Mary Masha kutoka Kenya na Ally Thabit kutoka Tanzania ambapo Mary Masha aliibuka mshindi kwa kura 21 kwa 15. Hivyo Rais wa wiki hii ni Mary Masha na malkia Elizabeth Simon.
Washindi waliopata kura sawa ni Mary Masha kutoka Kenya na Ally Thabit kutoka Tanzania ambapo Mary Masha aliibuka mshindi kwa kura 21 kwa 15. Hivyo Rais wa wiki hii ni Mary Masha na malkia Elizabeth Simon.
Utaratibu wa kuchagua wagombea: Kila mshiriki hujaza fomu kuteua jina la atakayekuwa kuwa Rais wa wiki hiyo. Walioteuliwa hujinadi ili wapate kupigiwa kura na hatimaye kupata mshindi.
↧
↧
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU BI ISABELA CHIRUMBA.
Na Wiliam Bundala matukiodaima kanda ya ziwa
Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama imewafuta kufanya kazi maofisa watendaji wa kata na vijiji wenye elimu ya darasa la saba kwa madai ya kuboresha ufanisi wa kazi zake baada ya kubaini wengi wao walikuwa wakifanya kazi kwa mazoea.Uamuzi huo ulithibitishwa hivi karibuni kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo ambayo imedaiwa hivi sasa hakuna ajira itakayotolewa kupitia mapendekezo ya Serikali za vijiji ambayo hupitisha watendaji kwa kujuana badala ya kufuata elimu na taaluma.
Katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichoongozwa na mwenyekiti wake Juma Kimisha kilipitisha uamuzi wa Maofisa watendaji hao waliopo kwenye mkataba wamalizie muda wao na baada ya hapo wajifute wenyewe kutokana na kukosa sifa ya elimu yakuwa watumishi wa Serikali.
Hata hivyo katika kikao hicho Madiwani hao nusura wapinge uamuzi huo uliodaiwa ni wa kisiasa baada ya kudai kuwafuta kazi watendaji wa darasa la saba ni kutowatendea haki kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu hali ambayo ilizua mvutano kwenye balaza hilo.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Egdius Kahendaguza aliwaambia Madiwani hao swala la kuwafuta watendaji hao lilishajadiliwa na kutolewa maamuzi katika vikao mbalimbali na tayari mkurugenzi wa Halmashauri alikwishatangaza nafasi za kazi kwa waliomaliza kidato cha nne.
↧
MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA KAHAMA MABALA MLOLWA
Na William Bundala(Kijukuu cha bibi k)
Wa Matukioo daima Kanda ya ziwa!!
Chama cha mapinduzi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kimewakumbuka mabalozi wake wa nyumba kumi kwa kuwaasa kuunda vikundi vya uzalishaji mali na kisha kuwapa mitaji ya kuanzia vikundi hivyo.
Katibu wa fedha na uchumi wa CCM wilaya ya Kahama Isaya Bukakiye amesema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha kitongo kwenye Halmashauri ya Ushetu ambapo alidai mabalozi wengi wao wamesahauliwa kiuchumi.
Katika mkutano huo Bukakiye amesema swala la baadhi ya viongozi wanaosaka nafasi za uongozi kuwajali wakati wa uchaguzi limepitwa na wakati lazima chama kama chama kiwatambue mabalozi katika umuhimu wao katika uhai wa chama.
Amesema umefika wakati sasa wa mabalozi hao kuacha kuitwa lugha ya kejeli na wapinzani kwamba ni makalai ambayo hukumbukwa wakati wa ujenzi peke yake ukikamilika hutupwa majalalani hali ambayo inaepukika iwapo mabalozi hao watawezeshwa miradi ya maendeleo.
Awali katibu wa siasa na uenezi wa kata ya Igwamanoni katika kijiji hicho cha kitongo Makoye Mahushi alimweleza kiongozi huyo wa chama kuwa hali ya uchumi kwa mabalozi ni ngumu ingawa ndio nguzo ya kwanza ya chama wakati wa uchaguzi.
Kufuatia hali hiyo Bukakiye aliwachangia shilingi milioni moja mabalozi wa kata ya Igwamanoni kwa ajili ya kuanzisha chama cha kuweka na kukopa SACCOS na kuahidi kuendelea kuwachangia kutokana na namna watakavyofanikiwa kuindeleza.
↧
PICHA 40 YA TUKIO ZIMA YA YALIYOJII KWENYE TUZO ZA KTMA 2014 USIKU WA KUAMKIA LEO:DIAMOND AVUNJA REKODI:
Add caption |
↧
SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI ILIVYOFANYWA KITAIFA JIJINI ARUSHA
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wakifanya usajili kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw. James Jesse, akitoa mada kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya uhuru wa kujieleza kwa kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yanayofikia kilele leo jijini Arusha.
Mwanahabari Mkongwe kutoka Chuo Kikuu Huria, Dokta Samwilu Mwaffisi (kulia) akiwasilisha mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Simon Berege.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akitoa maoni yake wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakongwe, mabalozi na wanahabari washiriki katika kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Mwandishi wa Habari Chokonozi, Bw. Fredrick Katulanda, akielezea madhila mbalimbali yaliyomsibu katika utekelezaji wake wa kuandika habari za uchambuzi.
Mwanahabari Mkongwe Bi. Leila Sheikh akichangia mada ya Mchango wa Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Katika Utawala Bora, Kukuza Uwezo Na Kupunguza Umaskini wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Mmiliki wa Gazeti tando la Mjengwa na Kituo cha Redio Kwanza Jamii, Bw. Maggid Mjengwa akielezea jinsi Intaneti inavyoweza kuunganisha mtandao wa Redio.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) na Mkurugenzi wa kituo cha mawasiliano Sengerema, Bw. Felician Ncheye akichangia mada.
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamamo hilo.
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Picha juu na chini Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 likiendelea.
Mwanakamati wa maandilizi ya maadhimisho ya Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda nje ya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
↧
↧
TRA YAWAPA SEMINA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA JUU YA MASHINE ZA EFDs
↧
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASMI SHEREHE ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI KAGERA







Mei 2, 2014. Mwenge huo unatarajia kuitimisha mbio zake Oktoba 14 mkoani Tabora, ambapo zinatarajia kufungwa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete. Picha na OMR
Baadhi ya wageni waalikwa, Wakuu wa Wilaya za mkoa ya Tanzania Bara na Visiwani, waliohudhuria sherehe hizo za uzinduzi.

Na: Aron Msigwa na Frank Shija- MAELEZO
BUKOBA
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal ametoa wito kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kufanya maamuzi yanayozingatia maslahi mapana ya taifa ili kufanikisha upatikanaji wa Katiba itakayokidhi matakwa na matarajio ya wananchi.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la kupiga kura ya maoni ili kufanikisha upatikanaji wa katiba shirikishi itakayoliongoza taifa kwa kipindi kirefu bila kuhitaji kufanyiwa marekebisho.
Akizindua Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2014 leo katika uwanja wa Kaitaba, manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Dkt. Bilal amesema mchakato unaoendelea wa upatikanaji wa katiba mpya ni jukumu la watanzania wote na kuongeza kuwa kila mwananchi analo jukumu la kuelewa mchango, wajibu na nafasi aliyonayo ili kukamilisha mchakato huu muhimu.
“Bunge Maalum la Katiba linaendelea na kazi kubwa, nachukua fursa hii kulipongeza kwa hatua linayoendelea nayo naamini maamuzi yote yatakayofikiwa yatazingatia maslahi mapana ya nchi yetu na kutoka na katiba inayokidhi matakwa ya wananchi” Amesema.
Amesema mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu zinabeba ujumbe muhimu usemao Katiba ni Sheria Kuu ya nchi chini ya Kauli inayowahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya maoni ili kuliwezesha taifa kuwa na Katiba mpya.
Dkt. Bilal ameeleza kuwa kila mwaka nchini mbio za Mwenge wa Uhuru huambatana na kauli ya kudumu kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, Rushwa , Dawa za kulevya na Malaria kwa lengo la kuwakumbusha wananchi kuendelea kupambana na chanagamoto hizo na kutafuta mbinu za kujikwamua .
Kuhusu changamoto hizo hususan ugonjwa wa Malaria amefafanua kuwa ni kati ya magonjwa yanayosababisha vifo kwa kiwango kikubwa hasa kwa akina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka 5 na kuongeza kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa huo sharti yapewe kipaumbele katika mbio za Mwenge kwa viongozi wa mbio hizo pamoja na mambo mengine kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo katika maeneo yote watakayopita kuanzia mwaka huu na kuendelea.
Ameeleza kuwa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa huo zinaonesha kwamba kati ya watu bilioni 3.3 sawa na nusu ya idadi ya watu duniani wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.
Amesema Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi za Bara la Afrika ambazo ugonjwa wa malaria ni moja ya magonjwa yanaoongoza kwa kusababisha vifo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 na wajawazito imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabilia na tatizo hilo.
“Kwa upande wetu serikali tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuifanya Tanzania bila Malaria iwezekane kwa wataalam wetu kuendelea kutoa ushauri na maelekezo kwa wananchi, kuimarisha upatikanaji wa dawa na huduma za matibabu katika hospitali zetu,kuhimiza matumizi ya vyandarua vyenye dawa, kuhimiza matumizi sahihi ya dawa za kuzuia malaria kwa akina mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 5”
Kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini Dkt. Bilal ameeleza kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kwa kushirikiana na jumuiya za kimataifa ili kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya VVU yanapungua na kufikia sifuri ifikapo mwaka 2015.
Akizungumzia mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya nchini amefafanua kuwa jukumu hilo linahitaji juhudi za pamoja kati ya serikali na wananchi na kueleza kuwa kwa upande wa serikali, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya inaendelea kutekeleza jukumu lake ili kuhakikisha Tanzania inakuwa salama.
“Tunatambua kuwa vita ya dawa za kulevye ni kubwa na inahitaji mchango wa kila mwananchi sote tunatakiwa kuungana na tume ili kuisaidia kutimiza majukumu yake”
Kwa upande wake waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akizungumza kabla ya uzinduzi wa mbio hizo amesema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikiwahamasisha wananchi kuibua, kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo wanayoishi.
Amesema kwa mwaka huu Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwa muda wa siku 165 katika Halmashauri za wilaya zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na zitahitimishwa mwezi Oktoba mwaka huu mkoani Tabora.
Kuhusu ujumbe wa mbio za Mwenge mwaka huu Dkt. Mukangara ameeleza kuwa unalenga kuwahamasisha wananchi popote walipo kushiriki kikamilifu katika mchakato wa katiba mpya ili kupata katiba bora kwa maslahi na mustakabali wa Taifa.
“Kwa kuwa katiba ndiyo sheria kuu ya nchi ni muhimu tukahakikisha kuwa kila mwananchi anatimiza wajibu wake wa kutoa uamuzi wa mwisho kwa njia ya kupiga kura ,nawahakikishia mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu zitafanya kazi hiyo ya kuwahamasisha wananchi kutimiza haki yao kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 ”
Naye Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe awali akizungumza wakati wa kuwakaribisha viongozi mbalimbali wa serikali, mabalozi, nchi washirika wa maendeleo na viongozi majirani wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Kagera zitaweka msisitizo mkubwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, Rushwa,Mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, uvunjifu wa amani na kila aina ya chuki na uhasama.
Amesema Mwenge wa Uhuru umeendelea kuwa chachu ya maendeleo ya taifa la Tanzania na kufafanua kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu ni za kipekee kutokana na umuhimu wake katika mkoa wa Kagera.
“Mwenge wa Uhuru ni chachu kubwa ya maendeleo utaleta matumaini, amani na heshima pale palipojaa dharalau na kwa hakika Mwenge huu utamulika na kuwafichua majambazi wenye silaha, wanaoishi nchini bila kufuata sheria, wezi wa mifugo, wanyanyasaji wa kijinsia, washirikina, waharibifu wa mazingira, wanaojichulia sheria mkononi, wavivu na walevi saa za kazi na wale wenye kuchochea migogoro ya dini na kabila” Amesisitiza.
Ameeleza kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2014 mkoani Kagera zitazindua utekeelezaji wa jumla ya miradi 69 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 69.
Amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika wilaya 7 za mkoa huo ambazo ni Biharamulo, Bukoba, Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Ngara kabla ya kukabidhiwa kwa viongozi wa mkoa wa Kigoma.
↧
SUMBAWANGA WAUA KIJANA ALIYEKUWA AKISAFIRISHA NYAMA YA WIZI
Na Elizabeth Ntambala matukiodaima.com Sumbawanga
Wananchi wenye hasira kali wamemuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Daniel ambaye alikuwa ni mkazi wa manispaa ya mjini sumbawanga katika mkoa wa Rukwa kwa kile kinachodaiwa kusafirisha nyama ya ng'ombe iliyokuwa imeibwa na watu wengine na ndipo marehemu aliponaswa na kukatwakatwa na shoka na mapanga ..Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Jacob Mwaruandaakitoa taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo (jana) nyakati saa tisa usiku katika kitongoji cha Malangali kilichopo mjini hapa.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kata ya Malangali, Baziri Stima, alisema kuwa chanzo cha kijana huyo kuuawa ni kutokana na kunaswa akisafirisha nyama ya ng'ombe kwa kutumia usafiri wa pikipiki yake ambayo ilibeba nyama hiyo ambayo ilichinjiwa katika mistu wa malangali hivyo kuhisiwa kuwa ng'ombe aliyechinjwa alikuwa wa wizi.
Inadaiwa kuwa baada ya kijana huyo kubeba mzigo wa kwanza, alirudia mzigo wa pili ndipo aliponaswa na kundi la watu na kuanza kuhojiwa alikoitoa nyama hiyo ambapo wakati akijaribu kutoa maelezo ghafla watu hao walianza kumshushia kipigo huku wakitumia silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na shoka hadi alipofariki dunia kisha kuichoma moto pikipiki yake.
Inaelezwa kuwa kuuawa kwa kijana huyo kufuatia kuwepo kwa matukio ya mara kwa mara ya wizi wa mifugo hususani ng'ombe ambapo wakazi wa kitongoji hicho wamekuwa wakilalamika kuibiwa mifugo yao na baadhi ya watu kisha ng'ombe hao kuchinjwa katika eneo la msitu wa malangali nyakati za usiku wa manane.
Kwa upande wa kamanda wa polisi mkoa huo, alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaina watu waliohusika na mauaji hayo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Mwaruanda alitoa rai kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi pindi wanapowakatama watu wanaowatuhumu kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu badala wawafikishe kituo cha polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
Hili ni tukio la pili la kijana wa bodaboda kuuawa baada ya kubeba nyama inayodaiwa ilitokana na wizi wa ng'ombe, tukio la kwanza lilitokea katika kata ya Senga ambapo kijana mmoja auawa na kuchomwa moto na watu wasiojulikana kutokana na kunasawa akisafirisha nyama hiyo.
↧